Mpayimana atangaza kuwania urais, Rwanda

Mpayimana Philippe anayeishi nchini Ufaransa, pia mwaandishi wa ‘’Refugees Rwandais entre le marteau et l’enclume’’ atangaza kuwania urais katika uchaguzi urais utakaofanyika mwaka huu wa 2017.

Mpayimana ,atakayekuwa mgombea huru katika uchaguzi, amesema kuwa si vizuri Kagame kukabidhiwa madaraka hadi achoke kwani Rwanda inahitaji mtu mwingine wa kuhifadhi umoja na maendeleo yaliyofikiwa.

Philipe Mpayimana ni mtu asiye toka katika vyama vinavyoiunga mkono RPR-Inkotanyi anayetangaza kuwania urais baada ya Dkt Frank Habineza kutoka chama cha kuhifadhi mazingira ‘’Green Party’’ aliyetangaza kuwania nafasi hiyo mwezi jana.
Uchaguzi urais unatarajia kufanyika tarehe 3, Agosti kwa wanyarwanda wanaoishi katika nchi za ugenini na tarehe 4, Agosti, 2017 kwa wanyarwanda wanaoishi ndani.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments