Polisi yaharibu pombe haramu zenye thamani ya Rwf 46 milioni

Jeshi la polisi linalofanya kazi mjini Kigali limeteketeza 200 kg ya bangi, maboksi 338 ya pombe haramu na kumwaga lita 115 za waragi vyenye thamani ya Rwf 46 milioni.

CSP Urbain Mwiseneza anaeongoza tawi linalopambana na madawa ya kulevya katika jeshi la Polisi amesema kuwa madawa ya kulevya yaliyoharibiwa ni yale aliyokamatwa katika msako uliofanywa ndani ya mji na mitaani inayoingia mjini.

Baada ya tukio hilo, Mwiseneza alishauri raia kushiriki na jeshi la polisi kwa kukomesha uuzaji wa madawa ya kulevya na pombe haramu.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments