Waziri mkuu wa São Tomé et Príncipe atembelea Rwanda

Rais Paul Kagame akiwa na mkewe Janet walitembelewa na Bw Patrice Emery Travoada akiwa na familia yake katika ikulu ya Rwanda, Village Urugwiro.

Waziri mkuu Travoada akiwa na mkewe Nana Travoada na watoto wao watatu walizuru makumbusho ya mauaji ya kimbari ya Gisozi mjini Kigali. Travoada alikumbusha dunia kuzuia kutokea tena kwa mauaji ya halaiki katika nchi yoyote ulimwenguni.

Patrice Emery Travoada ni mwanadiplomasia wa miaka 54 wa nchi hiyo inaopatikana kwenye upande wa Africa ya Magharibi aliyeteuliwa kuwa waziri mkuu tangu mwaka 2014 kwa mara ya pili.

Rais PaulKagame, Mkewe Janet katika picha na Bw Travoada na Nana Travoada pamoja na watoto wao watatu

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments