Watu wawili walifariki kwa kuporomokewa na ardhi

Watu wawili wamekufa na mwengine mmoja kujeruhiwa vibaya katika mkesha wa krismas.

Jeshi la polisi nchini Rwanda limeripoti kuwa Watu hao waliofariki dunia kwa kuporomokewa na ardhi katika vituo vya migodi vilivyopo wilayani Rubavu na Gasabo katika ajali mbili tofauti wiki jana.

Marehemu walikufa kwa kuporomokewa na vifusi wakati walipokuwa wakichimba migodi katika usiku kijijini cha Rushubi, kataa ya Gikombe, wilayani Rubavu.

Jean Paul Nzabandora aliyenusurika ajali lakini akajeruhiwa vibaya alipelekwa katika hospitali ya Kibagabaga anapopatiwa matibabu.

Modeste Mbabazi, Mkurugenzi wa tawi linalosimamia uhifadhi wa mazingira katika jeshi la polisi, ametoa wito wamiliki wa vituo vya migodi kulinda vituo vyao ili kuepuka uchimbaji haramu unaoweka hatarini maisha ya watu na alihamasisha wachimba migodi kuwa marafiki na mzingira.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments