Rufaa dhidi ya watuhumiwa wa mauji ya kimbari kusikilizwa mahakamani UK

Mahakama ya juu nchini Uingereza anasikiliza kwa upya kesi ya rufaa iliyowakilishwa na serikali ya Rwanda dhidi ya watu watano wanaoshitakiwa kushiriki mauaji ya kimbari dhidi ya raia wa kabila la kitutsi nchini Rwanda katika mwaka wa 1994.

Mwaka jana Mahakama ya Westminister magistrate lower court alitupilia mbali ombi lililotolewa na serikali ya Rwanda la kusafirisha nchini Rwanda Dkt Vincent Bajinya, Celestin Ugirashebuja, Charles Munyaneza na Emmanuel Nteziryayo ambao wote walikuwa mameya wakati wa mauaji ya kimbari kwa hofu ya kunyimwa haki ya kisheria baada ya kufikishwa mahakamani ya Rwanda.

Kesi hii inasikilizwa kwa upya kufuatia rufaa iliyotolewa na serikali ya Rwanda mahakamani ya Royal Court of Justice nchini humo dhidi ya washukiwa hao.
Hawa watano walikamatwa katika maeneo tofauti nchini Uingereza kutokana nyaraka za kuwakamata zilizotolewa na mahakama ya Rwanda.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments