Padri Thomas Nahimana akwama mjini Nairobi

Katibu mkuu wa Chama cha kisiasa kijulikanacho kama Ishema Party aliyetarajiwa kufika Rwanda jana alasifiri amekwama mjini Nairobi nchini Kenya kwa sababu ya kutokuwa na nyaraka za kusafiri.

Padri Thomas ni mnyarwanda aliyekuwa akifanya siasa barani Ulaya akisema kwamba yeye ni mpinzani wa uongozi wa chama tawala RPF-Inkotanyi.

Jana alikuwa akisubiriwa uwanjani wa ndege Kanombe na wadau wa habari lakini Tangazo kwa vyombo vya habari lililotolewa naye akiwa uwanjani wa ndege Jomo Kenyatta international Airport lilikuwa likisema kuwa yeye pamoja na wenzake wamekatazwa kuabiri ndage ya Kenya Airways kwenda nchini Rwanda kwani wao hawana nyaraka kamili za kusafiri.

Nchini Kenya Thomas Nahimana yuko pamoja na Venant Nkurunziza, mwnye umri wa miaka 33, Bi Claire Nadine Kasinge,36 na mtoto wake Kejo Skyler wa miezi saba.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments