Kigali : Watu wawili wameshikiliwa na Polisi kwa tuhuma ya kutumia fedha bandia.

Mtu mmoja wa miaka 55 na mwenzake wa miaka 31 wameshikiliwa na jeshi la polisi nchini Rwanda kwa tuhuma za kutumia fedha bandia.

SP Emmanuel Hitayezu ambaye ni msemaji wa jeshi la Polisi mjini Kigali aliambia magazeti kuwa mtu mmoja alikamatwa wilayani Nyarugenge akiwa na $500 na noti moja ya Rwf 2000.

Na mwingine alikamatwa wilayani Kicukiro akiwa na Rwf 38,000 mikononi na hawa wote wamefungwa vituoni vya polisi vilivyo karibu nao.

SP Hitayezu alisema kwamba polisi imeanza upelelezi wa kina ili kutambua chanzo cha hizi pesa.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments