Kampeni za kumtafuta seneta atakayechukua kiti cha Mucyo zaanza

Mucyo Jean de Dieu aliyefariki dunia mwezi jana

Akina mama watatu na wanaume wawili wametangaza nia yao ya kuwania nafasi bungeni/chumba cha maseneta iliyoachwa wazi na Mucyo Jean de Dieu baada ya kufariki Dunia mwezi jana.

Dkt Francois Masabo, Monique Mukakarera, Dkt Richard Sezibera, Veneranda Mukamuganga na Félicité Muhimakazi hawa ndio ambao wamepiga sauti zao juu wakisema kuwa wanataka kuwania kiti cha Mucyo ambaye alikuwa akiwakilisha Mkoa wa Kusini Bungeni. Charles Munyaneza, Katibu mtendaji wa tume ya uchaguzi amesema.

Kwa kawaida kuna maseneta 26, kumi na wawili wanachaguliwa kutoka mikoni mine ya Rwanda na municipaliti ya Kigali, wengine wanawakilisha makundi maalum , wakati wanne wanateuliwa na Rais.

Hii ndio sababu Wanakusini wanapaswa kumchagua seneta mwingine atakayejaza nafasi iliyoachwa wazi na Mucyo Jean de Dieu alifariki baada ya kuanguka ghafla Bungeni.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments