Katoliki yaomba msamaha kwa ushiriki wake katika mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi.

Dini ya kikatoliki nchini Rwanda iliwaombea msamaha waamini wake walioshiriki katika mauaji ya kimbari ya mwaka wa 1994 yaliyosababisha vifo zaidi ya mailioni vya watutsi nchini Rwanda.

Msamaha huo uliombwa katika barua iliyotiwa saini na maaskofu tisa katika jina la dini ya Kikatoliki nchini Rwanda na kusomewa mbele ya wakristo nchini kote siku ya jumapili iliyopita.

Barua inasema kwamba ingawa Dini ya Kikatoliki haijawahi kushiriki mauaji ya kimbari kama taasisi kwa ujumla , lakini wako wakristo wake waliotenda jinai la mauaji ya kimbari.

‘’ingawaje hakuna mtu ilioyetumwa na Katoliki kw kufanya mauaji, sisi maaskofu tunaomba msamaha kwa baadhi ya wakristo , wakuu wa dini, watu waliojitolea kwa kumtumikia mungu lakini wakakosa njia ya ujumbe waliopewa na mungu na wakatenda mauaji ya kimbari.’’

‘’Hao wote waliotenda dhambi hilo, tunawaombea mungu abadili nyoyo zao, awasaidie kutubu, kuishi katika amani na manusura na awape nguvu za kusema ukweli kuhusu yalitokea nchini Rwanda.’’

‘’sisi maaskofu, tunaomba msamaha kutokana na uhalifu mbalimbali uliofanywa na wakristo na wakuu wa dini ya kikatoliki, tunasikitishwa na wenzetu waliopuuza ujumbe wa mungu katika amri zake ubatizo kisha wakaua jirani na marafiki zao.’’

Askofu Philippe Rukamba wa dayosis ya Butare alisema kwamba wao waliandika tamko hili kwa kuonesha kuwa mauaji ya kimbari ni mpango uliopangwa na serikali iliyokuwa madarakani, Dini ya Kikatoliki hakukuwa uhusiano na mpango huo.

Dkt Jean Damascena Bizimana, katibu mtendaji wa tume ya kupambana na mauaji ya kimbari nchini Rwanda alisema kuwa uamuzi uliochukuliwa na Dini ya Kikatoliki ni uamuzi halisi unaostahili kuigwa na wengine.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments