Valens Ndayisenga aibuka mshindi wa Tour of Rwanda

Mashindano ya Tour of Rwanda yakamilika

Mnyarwanda Valence Ndayisenga ameibuka mshindi wa mashindano ya mbio za biaskeli ya Tour of Rwanda.Amembwaga bingwa wa Afrika Okumariam Tesfom kutoka Eritrea aliyeshinda mzunguko wa saba na wa mwisho wa mashindano hayo kwa kutumia muda wa saa 2 dakika 43 sekunde 21 akimshinda kwa tairi tu ya baiskeli mwenzake wa Eritrea Eyob Metkel ,huku Valence Ndayisenga akichukua nafasi ya tatu.

Hata hivyo kijana huyu mwenye umri wa miaka 22 ameibuka na ushindi wa Tour Of Rwanda kwa ujumla.

Kwa awamu zote 7 za mashindano haya alitumia muda wa saa 21 dakika 15 na sekunde 21 na kumshinda Eyob Metkel kukiwa na tofauti ya sekunde 39.
Hawa wanachezea timu moja ya Dimension Data ya Afrika Kusini. Bingwa wa afrika Okumariam Tesfom amechukua nafasi ya tatu.

Ni kwa mara ya pili Valence Ndayisenga akiibuka mshindi wa Tour Of Rwanda. Mara yake ya kwanza ilikuwa mwaka 2014 ambapo moja kwa moja alisajiriwa kama mwanabaiskeli wa kulipwa na timu ya Dimension Data.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments