Mwezi mmoja umepita, Mwili wa Kigeli VI bado haujazikwa.

Mwezi mmoja umetimia baada ya kutangazwa kwa kifo cha aliyekuwa mfalme wa mwisho wa Rwanda mwezi Oktoba, 16,2016 hospitalini iliyoko mjini Oakton, Virginia nchini Marekani.

Baada ya kifo chake, mengi yalisemwa kuhusu ni wapi atakapozikwa ; Rwanda au Uhamishoni(Marekani) ?

Rwanda iliahidi kutoa msaada wowote utakaohitajika kwa kuandaa mazishi ya Kigeli VI, baadaye familia yake ilienda Marekani kuleta mwili wake na kuthibitisha kuwa ni lazima mwili wa mfalme huyo uzikwe nchini Rwanda, taifa lake la kuzaliwa.

Licha ya hayo yaliyokuwa akiandikwa na familia hiyo, Boniface Benzige ambaye alikuwa msemaji wa Kigeli VI alitupilia mbali taarifa iliyoandikwa na familia ya mfalme ambayo huishi nchini Rwanda.
Taarifa hiyo ilikuwa ikisema kwamba mwili wa Marehemu utazikwa Nchini Rwanda katika Nyanza, kusini mwa Rwanda.

Akihojiwa na Sauti ya Amerika mwezi huu tarehe mosi, Benzige alisema kwamba mfalme atazikwa nchini Marekani kama alivyotaka wakati alipokuwa hai.

Je, Kigeli VI atazikwa wapi ? Rwanda au Uhamishoni ? Mpaka sasa siku ya mazishi ya mwili wa mfalme wa mwisho wa Rwanda bado haijatangazwa.

.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments