Rais Kagame na mkewe wako mjini Marrakech, Morocco

Rais Paul Kagame na mkewe Janet Kagame wako mjini Marakech, Nchini Morocco ambako walikoenda kuhudhuria mkutano kuhusu mabadiliko ya anga unaoendelea kufanyika mjini Marakech nchini humo.

Ni mara ya kwanza Rais Paul Kagame kuhudhuria mkutano huo uitwao COP22 akiwa na mkewe Janet.

Katika mkutano wa COP22 ulioanza tarehe 7 mwezi huu na unatarajiwa kumalizika tarehe 18,11,2016, washiriki wanatarajiwa kuchukua maamuzi yatakayosaidia kupungua joto la sayari hadi chini ya 1,5 degree celesius.
Nchini Morocco, Rais Paul Kagame yuko pamoja na Louise Mushikiwabo ambaye ni waziri wa mambo ya nje na ushirikiano, pia msemaji wa serikali ya Rwanda

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments