Hatutaki kuwa kama Bruguière – Waziri Mushikiwabo

Serikali ya Rwanda inasema kuwa iko tayari kutangaza vibali vya kukamatwa kwa wafaransa walioshiriki katika mauaji ya kimbari ya Rwanda dhidi ya raia wa kabila la Kitutsi katika mwaka wa 1994.

Lakini Louise Mushikiwabo, waziri wa mambo ya nje na ushirikiano, pia msemaji wa serikali ya Rwanda, amesema kwamba Rwanda haiendi kufanya jinsi Hakimu wa Ufaransa Jean Louis Bruguière alivyotoa vibali vya kukamatwa kwa maafisa wakuu wa Rwanda kinyume na sheria mwakani wa 2006.

Katika mkutano na waandishi wa habari jana alhamisi, Bi Louise Mushikiwabo alisema kwamba Rwanda iko tayari kuwafikisha mahakamani wafaransa waliotenda makosa ya kijinai nchini Rwanda wakati wa mauaji ya kimbari iwapo makosa ya kijeshi au ya kisiasa.

Mushikiwabo anayasema hayo baada ya tume ya kupambana na mauaji nchini Rwanda CNLG kutoa orodha ya maafisa 22 wa kijeshi wanaoshukiwa na serikali ya Rwanda kushiriki mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi.

Akisema kuhusu orodha iliyotolewa na CNLG, Bi Mushikiwabo alisema kwamba ile sio maana ya kushikiliwa kwa washukiwa, ni maana ya kuanza kwa mchakato wa kisheria.

‘’ile orodha inamaana kuwa wapo wanajeshi na wanasiasa wa Ufaransa walioshiriki mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda.’’

Yeye aliendelea kusema kwamba ile orodhi ni ya wanajeshi tu lakini wao wako tayari kutangaza na orodha ya wanasiasa wa ufaransa waliotenda makosa ya kijinai nchini Rwanda.

Alisisitiza kuwa Rwanda haitakubali mambo ya kudharauliwa na kuwa kama Bruguiere aliyeamka na akawashitaki wanajeshi wa RPF-Inkotanyi kuidungua ndege ya Juvenal Habyarimana, aliyekuwa rais wa Rwanda, pasipo kufanya upelelezi.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments