Rais Kagame ampongeza Donald Trump kwa ushindi wake

Rais Paul Kagame amempongeza rais –mteule wa Marekani Bw Donald Trump kwa ushindi wake wa kiti cha Urais.

Akitumia ukurasa wake wa Twitter, Bw Kagame amemuahidi kuendelea urafiki na Marekani.

‘’Hongera Donald Trump kwa kushinda, tunautazama uhusiano mzuri na uongozi mpya wa Marekani.’’

Leo hii Donald Trump ambaye amekuwa akiwakilisha chama cha Republican katika uchaguzi mkuu ameshinda kiti cha urais kwa kura 48% wakati Bi Hillary Clinton amepata kura 47%.

Rais Paul Kagame amepiga msururu nyuma ya Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza, Vladmir Putin wa Urusi, Yoweli Museveni wa Uganda na Dkt John Pombe Magufuli wa Tanzania waliomtakia Bw Trump kheli tele.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments