Makumbusho ya mauaji ya kimbari ya Rwanda kusajiliwa kuwa urithi wa Dunia

Bi Uwacu Julienne, waziri wa michezo na utamaduni nchini Rwanda, Dkt Diogene Bideri, msimamizi wa urithi katika UNESCO na Mechtild Roosler, mjini Kigali

Serikali ya Rwanda yaanza mchakato wa kusajili makumbusho ya mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi kuwa urithi wa Dunia.

Tume ya kupambana na mauaji ya kimbari nchini Rwanda CNLG inasema kuwa inalenga kufikapo mwaka wa 2018 makumbusho ya Gisozi, Bisesero na Nyamata kumalizika kusajiliwa kwenye orodha ya urithi wa dunia na shirika kimataifa la Elimu, Sayansi na utamaduni, UNESCO.

Dkt Jean Damascene Bizimana, mkuu wa CNLG anasema kwamba mchakato huyub unajadiliwa katika mkutano wa siku mbili wa watalaam wa kupambana na mauaji ya kimbari na wahadhiri wa vyuo vikuu mjini Kigali.

Uwacu Julienne amesema kwamba kusajiliwa kwa makumbusho ya mauaji ya kimbari ya Rwanda kutasaidia kujulikana kwa historia ya mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments