Mwanamke wa kwanza wa Benin awasili Rwanda

Mke wa Rais wa Rwanda, Bi Janet Kagame amempokea mwenzake wa Benin ziarani ya siku nne nchini Rwanda.

Bi Claudine Talon, mke wa Patrice Talon, amefika uwanjani wa ndege Kanombe jana jioni ya jumatatu ambapo alipokaribishwa na Janet Kagame.

Kwenye ajenda yake, Claudine Talon anatarijia kutembelea miradi inayofanywa na Imbuto Foundation, shirika lililoundwa na linaloongozwa na Janet Kagame.

Na akiwa na mwenzake wa Rwanda, Claudine atazungumziwa kuhusu shughuli zinazolenga kuimarisha elimu, uchumi na ustawi wa jamii kwa ujumla.

Leo hii, Bi Claudine anatembelea Isange One Stop Center na makumbusho ya mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi hapo Gisozi.

Bi Claudine Talon anazuru Rwanda baada ya mmewe Patrice Talon kutembelea Rwanda mwezi Septemba, mwakani huu.

Bi Claudine Talon akituwa Kanombe, mjini Kigali

Akifika, Claudine alipokewa na Janet Kagame

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments