Mfanyabiashara Makuza Bertin afariki

Makuza Bertin akiwa na Rais Paul Kagame wakati wa ufunguzi wa M Peace Plaza

Mmoja wa wafanyabiashara maarufu nchini Rwanda Makuza Bertin amekufa katika usiku wa kuamkia leo hii, tarehe 3, Novemba,2016.

Taarifa zinasema kuwa Bertin hapo jana aliamka akiwa na maisha mazuri na hata siku za nyuma yeye hajapata ajali wala kulazwa hospitalini kuugua maradhi yoyote.

Lakini wakati alipokuwa katika gari lake akitembea, aliomba dereva wake kumpeleka hospitalini kwa sababu alikuwa anahisi vibaya, moja kwa moja aliwasilishwa hosptalini ya King Faisal iliyoko mjini Kigali ambapo alipokata roho.

Ripoti zinasema kwamba Bertin amefariki kwa uchovu. Makuza Bertin ndiye mmiliki wa kiwanda cha RwandaFoam ,kinachozalisha magodoro na jengo kubwa liitwalo M Peace Plaza.

Marehemu Makuza Bertin

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments