Rwanda yalishutumu jeshi la Ufaransa kushiriki mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi

Tauzin (kushoto) Lanxade na Hoggard wanaoshtakiwa kushiriki mauaji ya kimbari na ripoti ya CNLG

Tume ya kupambana na mauaji ya kimbari nchini Rwanda CNLG imechapisha ripoti inayolishutumu jeshi la Ufaransa kushiriki mauaji ya kimbari ya mwaka wa 1994 dhidi ya raia wa kabila la Kitutsi.

Ripoti hii imeyataja majina 22 ya maafisa wa kijeshi wa Ufaransa wanaoshtakiwa na serikali ya Rwanda kushiriki na kufadhili uongozi wa Habayarimana kutenda mauaji ya kimbari yaliyosababisha vifo zaidi ya milioni vya watutsi nchini Rwanda.

Majina yaliyotajwa ni Jenerali .Jacques Lanxade, Jenerali. Christian Quesnot, Jenerali. Jean-Pierre Huchon, Lt kanali. Michel Robardey , Kanali. Gilbert Canova, Kanali Grégoire De Saint Quentin, Kanali Dominique Delort, Lt.Col Jean-Louis Nabias na Col Denis Roux, na mengineyo.

Ripoti hii inaeleza kwamba hawa walikuwa maafisa wa kijeshi wa Ufaransa waliotumwa nchini Rwanda kutoa msaada wa aina yote kwa uongozi wa Juvenal Habayarimana wakati wa mauaji ya kimbari.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments