Jeshi la Rwanda limetupilia mbali madai ya kumuua mvuvi raia wa Burundi

1

Luteni Kanali Rene Ngendahimana, msemaji wa majeshi ya Rwanda
Jeshi la Rwanda lemetupilia mbali habari zilizokuwa zikisema kwamba askari wa Rwanda walimfyatua risasi na kumuua mvuvi raia wa Burundi jumamosi iliyopita ziwani Rweru.

Gavana wa mkoa wa Kirundo unaopakana na Rwanda katika sehemu ya kusini, Melchior Nankwahomba aliambia gazeti la wachina kuwa Mrundi mmoja aliuawa na jeshi la Rwanda na mwingine kutekwa nyara.

Lakini, Luteni Kanali Rene Ngendahimana, msemaji wa majeshi ya Rwanda, akiongea na igihe, alisema kwamba hayo ni uongo mtupu.

‘’hakuna mtu aliyepigwa risasi na majeshi ya Rwanda, watu walipatikana karibu na mpaka wa Rwanda ziwani Rweru jumamosi asubuhi, kama vilivyokuwa askari wa Rwanda ambao walikuwa wakishika doria walipiga risasi hewani na kuwaomba kujisalimisha.’’

Yeye alieleza kwamba wanajeshi wa Rwanda walipiga risasi hewani kwa kuwaonya, mmoja wapo alikuja juu na akaongea na askari bila uoga, wenzake walichagua kukimbia ; hakuna askari aliyewafuata.

‘’Hakuna mtu aliyeuawa, majeshi ya Rwanda walipiga risasi hewani kwa kuwataka warudi nyuma au wasogee mbele kwa kujieleza.’’

Luteni Kanali Ngendahiamana alisisitiza kwamba hakuna mtu aliyeuwa na madai hayo ni uongo unaotumika na Burundi kwa kuchafua sifa ya Rwanda.

Changia hii habari na wenzako.

Comments 1

  1. enyi warundi,jaribuni kutoona jeshi la Rwanda kama wa saliti wa usalama wa raia zenu.bali sikieni kwamba wako kwenye ulinzi kwa manufaa ya taifa zote mbili kama nchi jirani

Tumia Comments