Rais Kagame awasili Gabon

Rais wa Rwanda, Bw Paul Kagame amewasili nchini Gabon ziarani rasmi ya siku mbili za kazi.

Akiandika kwenye ukurasa wake wa twitter, Rais Ali Bongo Ondimba wa Gabon alisema kwamba anafurahi kwa kumpokea Bw Kagame nchini mwake.

‘’ nimempokea ndugu na rafiki yangu Paul Kagame kwa furaha nyingi katika ziara ya siku mbili.’’

Bw Ondimba aliongeza kwamba ziara ya Rais Kagame nchini ,mwake ni fursa ya kuimarisha ushirikiano baina ya nchi mbili na kuyajadili maswala mengi yakiwemo kilimo, uchumi, mazingira,...

Rais Paul Kagame analizuru taifa la Gabon baada ya kuyatembelea mataifa ya Msumbiji na Jamhuri ya Kongo majuzi.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments