APR FC na Rayon Sports kurudi uwanjani kwenye siku ya tatu ya ligi kuu

Muhadjili Hakizimana,kushoto, atakuwa akicheza dhidi ya Mukura VS(Timu aliyeichezea mwaka jana
Rayon sports na APR FC, timu kubwa katika historia ya kandanda nchini Rwanda ukulinganisha na wenzao, zinatarajiwa kurudi uwanjani kwenye siku ya tatu ya Ligi kuu ya Rwanda msimu wa 2016-2017.

Rayon sports itarudi uwanjani siku ya jumapili dhidi ya AS Kigali na APR FC inachuana dhidi ya MukuraVS leo hii ya ijumaa, uwanjani wa Kigali/Nyamirambo.

Baada ya siku mbili za msimu huu, Etencilles na Sunrise zinaongoza meza ya ligi zikiwa na alama 6 kila mmoja.

Michezo mingine

Ijumaa, tarehe 28, oktoba,2016

APR FC vs Mukura VS (uwanja wa Kigali, 18:00)

Jumamosi

Sunrise Fc vs Marines Fc (Kicukiro, 15:30)
Bugesera Fc vs Espoir Fc (Bugesera, 15:30)
SC Kiyovu vs Gicumbi Fc (Mumena, 15:30)
Pépinière Fc vs Kirehe Fc (Ruyenzi, 15:30)

Jumapili

Etincelles vs Musanze Fc (Umuganda, 15:30)
Amagaju Fc vs Police Fc (Huye, 15:30)
Rayon Sports vs AS Kigali (Stade ya Kigali, 15:30)

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments