Shirkisho la kabumbu kumtangaza kocha mkuu wa timu ya taifa mwaka ujao

Shirikisho la kandanda nchini Rwanda limetangaza kuwa hakuna maana ya kuajiri kocha mpya wa timu ya taifa wakati hakuna mashindano kimataifa wanaojiandaa kucheza mwaka huu.

Nzamwita Vincent De Gaulle, mkuu wa FERWAFA, ameliambia gazeti la the Newtimes kwamba wao hawajaoni umuhimu wa kuteua kocha mpya wa Amavubi Stars wakati Amavubi wanatarajia kushuka dimbani tena angalau mwezini Mei, 2017.

Vincent Nzamwita aliongeza kuwa timu ya taifa itarudi uwanjani mwezi Juni, 2017 wakati wa kusaka tiketi ya kufuzu michezo ya kombe la Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN).

Jonathan McKinstry, mwiingereza aliyekuwa kocha mkuu wa Amavubi Stars alitimuliwa kwa kosa la kutoifuzu timu ya taifa katika mashindano ya kombe la Afrika atakaofanyika nchini Gabon mwaka ujao.

Na baada ya Rwanda kupata nafasi ya aibu kwenye viwango vya FIFA.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments