Rais Magufuli atajwa kuwania tuzo ya mtu mashuhuri wa mwaka

JARIDA maarufu la Forbes la nchini Marekani, limemtaja Rais Dk. John Magufuli, kuwania tuzo ya Forbes ya Mtu Mashuhuri wa Mwaka Afrika.

Rais Dk. Magufuli ametajwa na Jarida hilo la biashara kwa kutambua umuhimu wake katika kuimarisha uchumi wa Tanzania.

Rais Dk. Magufuli anachuana na watu wengine wanne kuwania tuzo hiyo wakiwemo ; Rais wa Mauritius, Ameenah Gulib, Mwanzilishi wa Benki ya Capitec, Michiel Le Roux na mwanasheria na mtetezi wa haki za binadamu nchini Afrika Kusini, Thuli Madonsela pamoja na watu wa Rwanda.

Mwaka jana, 2015 Mfanyabiashara Mohammed Dewji wa Tanzania alishinda tuzo hiyo, huku bilionea namba moja Afrika, Aliko Dangote akiwa ndiye mshindi wa mwaka 2014.

Wengine ni Akinwumi Adesina wa Nigeria mwaka 2013, James Mwangi wa Kenya mwaka 2012 na Sanusi Lamido Sanusi wa Nigeria mwaka 2011, ambao tuzo hizo zilizinduliwa.

Hadi sasa Rais Dk. Magufuli anaongoza kwa asilimia 84 akifuatiwa na watu wa Rwanda asilimia 12 huku zikiwa zimebaki siku 22 tu za kupiga kura mtandaoni.
Tuzo hizo kwa mwaka huu zitatolewa jijini Nairobi, Kenya Novemba 17.

Utaratibu wa jinsi ya kupiga kura kwa mwaka huu ni kutumia tovuti ya http://poy2016.com/ ambapo baada ya kuingia hapo, unaweza kugusa jina la mtu ambaye unapendekeza ashinde tuzo na hapo kura itakuwa imehesabiwa.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments