Rwanda yashika nafasi ya pili barani kwa kurahisisha uwekezaji. – Ripoti

Ripoti mpya ya benki ya Dunia (the 2017 world doing business report) imeorodheshwa Rwanda kwenye nafasi ya pili barani Afrika na ya 56 ulimwenguni nzima miongoni mwa mataifa yanaorahisisha uwekezaji, ikifuata na visiwa vya Mauritius.

Barani Afrika, Botswana imetajwa kwenye nafasi ya tatu, Afrika kusini ya nne na Morocco ya tano.

Ripoti hii ya benki ya Dunia ni mojawapo wa ripoti zinazofanywa kila mwaka kwa lengo la kuonesha pingamiza zinazokabilia biashara ulimwenguni.

Kwa kuorodhesha mataifa, Ripoti hii inajikita kuhusu jinsi mataifa yanayorahisisha huduma kwa wanaotaka kuwekeza kama kupata vyeti vya ujenzi, upatikanaji wa umeme, viwango vya kodi,..

Rwanda inasifika kwa kutumia teknolojia katika nyanja ya biashara, ikiwemo ulipaji kodi na kujisajili.

Ripoti hii haikusahau usawa wa kijinsia unaopatikana nchini kwa ujumala na hasa katika biashara. Hivi ndivyo vilivyoifanya Rwanda kupata nafasi ya 2.

Francis Gatare, mkurugenzi wa bodi ya maendeleo (RDB), amesema kuwa ripoti hii imeonyesha jitihada muhimi ambazo nchi inatumia kwa kuwasaidia wafanyabiashara kuendesha biashara zao.

Iradukunda Desire

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments