Rais Kagame anasubiriwa nchini Usumbiji

Rais Paul Kagame anasubiriwa nchini Usumbiji katika ziara ya kikazi itakayoanza leo hii ya Jumatatu tarehe 24, Oktoba, mwaka huu hadi tarehe 25 kama vilivyo tangazwa na Louise Mushikiwabo, waziri wa mambo ya nje na ushirikiano, pia msemaji wa serikali, akiwa mjini Maputo nchini humo.

‘’Mimi niko katika Usumbiji kwa sababu ya kujiandaa ziara ya Rais Paul Kagame , nimefurahi sana kwa kuwaona wanyarwanda wanaoishi hapa Usumbiji.’’ Mishikiwabo alisema.

Yeye aliendelea kusema ziara hii ya Bw Kagame inalenga kuimarisha ushirikiano baina ya nchi mbili.

‘’ujio wa Paul Kagame ambayo utaanza tarehe 24-25 unalenga kujadili maswala mengi yakiwemo uimarishaji wa kilimo, uvuvi, miundombinu, sheria na kadhalika.’’ Louise aliongeza.

Gazeti la Club of Mozambique limeandika kwamba Paul Kagame anatarajia kutoa hotuba kuhusu mchango wa uwekezaji kwa kuendeleza nchi kwamba katika ukumbi wa Joaquim chissano international conferencxe center, mjini Maputo.

Rwanda inasifiwa kurahisisha uwekezaji ambapo inashika nafasi 62/189 ulimwenguni nzima kwa mujibu wa viwango vya Doing Busness.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments