Oda Gasinzigwa na mwenzake wa Burundi waapishwa kuwa wabunge katika EALA

Bi Oda Gsinzigwa
Oda Gasinzigwa aliyechaguliwa na bunge kuiwakilisha Rwanda katika bunge la jumuiya ya Afrika ya Mashariki na Jean Marie Muhirwa atakayeiwakilisha nchi ya Burundi waapishwa rasmi kama EALA inavyotangaza.

Oda na Jean Marie walitoa viapo vyao jana kwenye makao makuu ya EALA aliyopo Nchini Tanzania na viapo vilipokewa na Daniel F. Kidega ambaye ni mwenyekiti wa bunge.

Oda Gasinzigigwa alichukuliwa nafasi ya Christophe Bazivamo, aliyeteuliwa kuwa makamu wa katibu mkuu wa EAC.

Na Jean Marie Muhigwa alichukua nafasi ya Marehemu Afsa Mossi alifariki dunia mwezi Julai,2016 kwa kupigwa risasi mjini Bujumbura.

Muhirwa Jean Marie anayewakilisha Burundi ni mwanchama wa CNDD-FDD, Bi Oda Gasinzigwa ni mwanachama wa chama tawala nchini Rwanda RPF-Inkotanyi.

Muhirwa Jean Marie anayeiwakilisha nchi ya Burundi katika EALA.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments