Mfalme wa Morocco atoa heshima kwa wahanga wa mauaji ya Kimbari

Mfalme Mohammed VI na Dkt Vincent Biruta, waziri wa maliasili
Jana, Mfalme Mohammed VI wa Morocco atoa heshima kwa wahanga zaidi ya 25,000 wa mauji ya kimbari dhidi ya Watutsi waliozikwa makaburini ya Gisozi ‘’Gisozi Genocide Memorial centre’’.

Katika ujumbe wake alioandika katika kiarabu, Mohammed VI alisema kwamba mauaji ya halaiki alikuwa janga kwa binadamu na litaendelea kuwa changamoto kwa mwanadamu.

‘’Rwanda ya leo inajijenga kimaisha ; ina imani kwa sasa na siku zijazo ambapo umoja, usalama na utulivu ni vipaumbele’’ Mfalme aliandika katika Kiarabu.

Huko Gisozi, Mfalme alikuwa pamoja na mawaziri wawili wa Rwanda ambao ni Uwacu Julienne, waziri wa michezo na Utamaduni, Dkt Vincent Biruta, waziri wa maliasili.

Pia, alikuwa pamoja na Katibu mtendaji wa tume ya taifa ya kupambana na mauaji ya kimbari, Dkt Jean Damascene Bizimana.

Kwa kutoa heshima kwa wahanga wa mauaji ya kimbari, Mohammed VI aliweka shada la maua juu ya kaburi ya wahanga wa mauaji ya kimbari ya mwaka wa 1994 dhidi watutsi .

Wakati wa ziara yake ya siku tatu nchini Rwanda , Rwanda na Morocco walisaini makubaliano 19 hususan kwa kuimarisha ushirikiano, utalii, kilimo, uwekezaji baina ya nchi mbili.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments