Oda Gasinzigwa achaguliwa kuwakilisha Rwanda katika EALA

Aliyekuwa waziri wa mipango ya familia na usawa wa kijinsia Bi Oda Gasinzigwa achaguliwa kuwa mbunge atakayewakilisha Rwanda katika bunge la Afrika Mashariki, EALA.

Oda Gasinzigwa amechukuliwa nafasi alioachwa wazi na Bazivamo Christophe baada yeye kuchaguliwa kuwa makamu wa katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Gasinzigwa amechukuliwa nafasi na Bunge la Rwanda baada ya kumshinda Bw Kananugire Callixte,mtumishi wa sekretarieti ya chama tawala RPF-Inkotanyi, kwa wapiga kura 71 kwa wanne tu waliomchagua Bw Callixte.

Bi Oda Gasinzigwa ni mwanachama wa RPF-Inkotanyi na aliwahi kuhudumu kama waziri wa mipango ya familia na usawa wa kijinsia nchini Rwanda, MIGEPROF.

Bi Oda na Kanamugire Callixte wamekuwa wagombea kwenye nafasi ya kuwakilisha Rwanda katika EALA

Uchaguzi umeonyesha kwamba Oda Gasinzigwa ndiye mshindi

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments