Mfalme wa Morocco kutua Rwanda

Mfalme Mohammed VI wa Morocco anasubiriwa nchini Rwanda leo tarehe 18, Oktoba,2016 katika ziara ya siku mbili ya kazi kabla ya kuelekea Tanzania na Ethiopia.

Mohammed VI anatembelea Rwanda baada ya Rais Paul Kagame kumtembelea katika ufalme mwake mwezi Juni,20 ambapo walijadili uimarishaji wa ushirikiano baina ya nchi mbili na kumvisha Kagame medali ya heshima.

Ziara hii itakuwa fursa kwa mfalme wa Morocco kualika wakuu wa mataifa kwa kuhudhuria mkutano kuhusu mabadiliko ya anga utakaofanyika nchini Morocco mwezi Novemba,7-18,2016 kama magazeti nchini Morocco anavyoandika.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments