Rais Kagame atangaza kustaafu kwa Jenerali na afisa mwingine wa jeshi la Rwanda

Meja Jenerali Richard Rutatina
Akitumia nafasi yake kama Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Rais Paul Kagame awatangazia mawaziri kwamba yeye amekubali kustaafu kwa Meja Jenerali Richard Rutatina na Meja Issa Karamage.

Hayo yametangazwa katika Mkutano maalum wa mawaziri uliofanyika jumatano tarehe 12,Oktoba, 2016 katika ikulu ukiongozwa na Rais Paul Kagame.

Meja Jenerali Richard Rutatina amestaafu baada ya kupoteza nafasi ya mkuu wa ujasusi wa kijeshi, mwezi Februari.

Richard Rutatina aliwahi kuhudumu kama mshauri wa Rais Paul Kagame kuhusu mambo ya usalama na ulinzi.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments