Wanajeshi 3 wafariki na wengine 21 wamejeruhiwa katika ajali ya gari la kijeshi

Jana Mwezi Oktoba,11,2016 Gari la kijeshi lilifanya ajali katika Wilaya ya Kicukiro, tarafa ya Niboyi mjini Kigali.

Wanajeshi watatu waliripotiwa kufariki dunia na wengine 21 kujeruhiwa kama Msemaji wa jeshi la Rwanda alivyosema.

Na Luteni Kanali Rene Ngendahimana aliongeza kuwa miongoni mwa 21 waliojeruhiwa wamo 6 waliojeruhiwa vibaya.

Gari hili ambalo lilikuwa kutoka Nyanza ya Kicukiro kuelekea Kicukiro Centre lilikosa barabara baada ya dereva kuepuka kugonga gari la abiria kisha gari la kijeshi likaanguka nje ya barabara.
Habari nyingine yenye uhusiano na habari hii ya ajali

http://sw.makuruki.rw/spip.php?article3099

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments