Rwanda yawashutumu mabalozi wawili wa Ufaransa kushiriki katika mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi.

Dkt Jean Damascene Bizimana, katibu mtendaji wa Tume ya Kupambana na mauaji ya kimbari nchini Rwanda.

Utafiti uliotolewa na tume ya kupambana na mauaji ya Kimbari nchini Rwanda (CNLG) unawashutumu mabalozi wawili waliowakilisha nchi ya Ufaransa nchini Rwanda miakani ya 1990-1994.

CNLG inasema kwamba Martres Georges aliyewakilisha Ufaransa nchini Rwanda tangu mwakani wa 1989-1993 na Jean Michel Marlaud aliyewakilisha Ufaransa tangu 1993-1994 walikuwa wakifuatilia karibu michakato ambayo ilikuwa kupangwa hadi kuwepo kwa mauaji ya kimbari ya mwaka wa 1994 dhidi ya kabila la kitutsi.

Utafiti huo unasema kuwa Martres Georges alikuwa akijua kinachoendelea na kuisaidia serikali ya chuki kutimiza mauaji na Georges alikubali mbele ya wabunge kwamba yeye alijua kuwa mauaji ya kimbari alipaswa kuwepo mwishoni mwa 1990.

‘’[….]tangu ya wapiganaji wa RPR-Inkotanyi kuishambulia Rwanda, Raia wa kabila la Kihutu walianza kushawishi mauaji ya kimbari. Kanali Serubuga, naibu mkuu wa majeshi, alisema kwamba shambulizi la RPF ni sababu ni sababu tosha ya kuua watutsi .[…] tangu mwaka wa 1990 watu wengi wa kabila la Kitutsi walianza kufungwa kwa sababu wao walikuwa watutsi tu.’’ Martres alinukuliwa.

Jenerali Jean Varret, kiongozi wa mahusiano ya kijeshi tangu 1990- Aprili,1994 baina ya serikali ya Juvenal Habyarimana na Ufaransa, aliambiwa na Rwagafilita Pierre Celestin, aliyekuwa mkuu wa vikosi vya usalama, kwamba ‘’watutsi ni wachache, tutawaangamiza.’’

Kuhusu Marlaud Jean- Michel, CNLG inasemakwamaba yeye alisifu uongozi wa chuki, akishirikiana na vyama vyenye msimamo wa kikabila.

Marlaud mbele ya wabunge alisema kuwa alijua habari zote zilikuwa zikionesha dalili za mauaji ya kimbari .

CNLG inasema kuwa iliona ujumbe ufupi ambayo mabalozi walituma Paris na hotub na taarifa za kidiplomasia zinazoonyesha kwamba wao walisaidia serikiali ya wauaji wakati walish jua kwamba ulikuwa ukianda mauaji ya kimbari dhidi ya kabila la Kitutsi.

Na baada ya mauaji ya kimbari, Mabalozi walisaidia wauaji kutoroka na kukana mauaji ya kimabari dhidi ya watutsi katika matamshi yao.

Hatimaye, CNLG ilithibitisha bila shaka, hawa mabalozi wawili walikuwa wakijua mpango wa kuangamiza watutsi uliokuwa ukipangwa na serikali ya Juvenal Habyarimana.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments