Muungano wa Ulaya umeunga mkono pendekezo la kurekebisha itifaki ya Montreal

Tina Birmpili na Philip Owen, mkuu wa tume ya Muungano wa Ulaya
Tume ya muungano wa Ulaya imetoa msaada kifedha sawa na €250,000 kama dalili ya kueleza jinsi wanavyounga mkono pendekezo la kurekebisha itifaki ya Montreal,ya kukingia Ozoni, yaliyosainiwa mwaka wa 1987 .

Tina Birmpili, Katibu mtendaji wa Ozoni Skretarieti na mkuu wa wajumbe wa Umoja wa Ulaya wamesaini dili hii ili kusadia shughuli za kukomesha hewa chafu ya Hydrofluorocarbons hadi mwishoni mwa mwaka wa 2017 kama taarifa inavyosema.

Taarifa inasema kwamba huo mchango wa kifedha umetolewa baada ya kikao cha washirikiwa mkutano kuhusu kurekebishwa kwa makubaliano ya Montreal unaoendelea kufanyika mjini Kigali.

Kwa mjibu wa taarifa, pesa hizi zitatumika kwa kusaidia shughuli zitakazo lenga kuendeleza mipango ya kutokomesha hewa chafu ya Hfcs.

‘’tangu mwanzo, muungano wa ulaya umeunga mkono pendekezo la kurekebisha itifaki ya Montreal, na huu msaada unaonyesha jitihada zao za kupambana na mabadiliko ya anga.’’ Taarifa inasema.

‘’ mchango huu ni hatua muhimu utakaosaidia mengi na uanonyesha hamu ya tume ya ulaya ya kuhakikisha michakato yote.’’ Birmpili alisema.

Montreal Protocol Meeting unafanyika mjini Kigali tangu Oktoba,8-14 katika jingo la Kigali Convention Center.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments