Viongozi wamlimbikizia sifa Seneta Mucyo.

Viongozi wakuu nchini Rwanda wamemsifu waziri wa zamani wa sheria Jean de Dieu Mucyo ambaye anazikwa leo siku nne baada yake kufariki akiwa umri wa miaka 55.

Jeneza lenye mwili wa Mucyo limebebwa bungeni ambapo viongozi kadhaa wakiwemo Rais Paul Kagame wametoa heshima zao za mwisho kabla ya mwili wake kuelekezwa mazishini Rusororo.

-  Ujumbe wa Rais Paul Kagame uliosomwa na Bi Venantie Tugireyezu, waziri katika ikulu, amesema kwamba Rwanda imepoteza mtu muhimu.

-  Makuza Bernard, mkuu wa seneti, amesema kuwa kifo cha seneta Mucyo ni hasara kubwa katika familia na taifa ‘’kifo cha Mhe. Mucyo Jean de Dieu ni hasara kubwa katika familia yake, seneti na nchi yote kwa ujumla, tumempoteza mtu muhimu na mtu mwenye rehema.’’

‘’ na sisi maseneta tuko familia yake, tuataendelea kuwa karibu na familia yake kama alivyofanya kwa wengi.’’ Makuza aliongeza.

-  Katibu mkuu wa chama tawala FPR-Inkotanyi, Francois Ngarambe amesema kwamba mashujaa hawafariki na Mucyo ni shujaa ; yeye atakuwepo daima.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments