Ndoa haramu kuzusha matata, Nyagatare

2

Wilayani Nyagatare tarafa ya Karangazi mabibi wanalamikia kuhatarika vibaya baada ya kufanya arusi haramu na mabwana zao kinyume na sheria.

Hawa wamama wanashitaki wafunga ndoa wao matumiza ya mali za familia ambapo wanaume wanapozichukua kwenda kula raha wakati familia zao zinakumbwa na mateso kadhaa.

Hawa wanadai kwamba hili ni suala linalojitokeza mara nyingi katika familia za watu wasio asili ya Nyagatare kama mwandishi wetu aliyeko Nyagatare alivyojionea.

Hawa wanawake wanasema kwamba wao wanadanganywa kufunga ndoa kisheria lakini baada ya siku chache wakifunga ndoa, wanaume wao wakawaacha kama ganda la mnazi.

Uwihoreyimana ni mmoja wao, yeye alisema kwamba bwana wake alimuacha wakiwa na watoto wawili ambako mmewe alikwenda akibeba na vyote walivyopata wakiwa pamoja.

‘’mimi nilikubaliana na aliyekuwa mme wangu kufunga ndoa kisheria lakini baada ya kujifungua watoto wawili alishika mbuzi mbili tulizonunua, baskeli na mazao ya kilimo tuliyovuna na akaenda, nilibaki mikono mitupu na hao watoto wawili tu.’’ Uwihoreye alisema.

Kwa upande mwingine, washitakiwa wanalalamika kwamba sababu ya kujitenga na wanawake wao ni kutokana na suala la usumbufu.

‘’unakutana na mschana mmaskini mkaanza kuhudumiana kimapenzi hatimaye mkafunga ndoa alafu akaanza kukusumbua, ukajiuliza sasa nfanyeje ? Baadaye ukamua kujitenga naye ili kujitafutia utulivu.’’
Nsabimana, mmoja wa wanaume alisema.

Hata hivyo, viongozi wa vijiji wameapa kufanya iwezekanavyo kwa kutatua suala hilo.

Sabiti Jean Bosco, mkuu wa kijiji cha Gakoma huko wilayani Nyagatare alisema kwamba suala hili linaenda kujadiliwa katika Umugoroba w’ababyeyi ambako maswala ya familia kama hayo yanazungumziwa.

Na uongozi wa wilaya amekubali kuwa suala hilo linafamika, Meya wilayani humo anayesimamia ustawi wa jamii amesema kwamba suala hilo linatokana na fikra mbaya kuhusu usawa wa kijinsia
na aliongeza kwamba kwa kulishughulikia suluhu wao wanaenda kuimarisha umuhimu wa Umogoroba w’ababyeyi.

Desire Iradukunda
.

Changia hii habari na wenzako.

Comments 2

Tumia Comments