Kagame anapokea viapo vya mawaziri wapya, makatibu na magavana.

Waziri Johnston Busingye, waziri wa sheria, Francis Gatare, mkurugenzi wa bodi ya Maendeleo na Claver Gatete, waziri wa fedha na mipango ya serikali wakati walipokuwa wakiapa ; mwezi Julai,24,2014

Leo Alhamisi, Oktoba,6,2016 Rais Kagame anapokea viapo vya mawaziri,makatibu wa serikali na magavana waliochukuliwa nafasi mpya katika serikali ya Rwanda kama katiba inavyotarajia.

Jumanne iliyopita, Rais Paul Kagame aliteua viongozi wapya wakiwemo Nyirasafari Esperance aliyeteuliwa kuwa waziri wa mipango ya familia na usawa wa kijinsia (MIGEPROF) na Dkt Diane Gashumba aliyeteuliwa kuwa waziri wa Afya kutoka MIGEPROF.

Wengineo wapya walioteuliwa nyadhifa katika serikali ni Me Uwizeyimana Evode aliyechukuliwa nafasi ya kuwa katibu wa serikali katika wizara ya sheria kama mjibika wa katiba na sheria nyingine,

Munyeshyaka Vincent,katibu kudumu wa serikali katika wizara ya mitaa anasimamia ustawi wa jamii, Munyakazi Isaac, katibu wa serikali anayesimamia mashule ya sekondari na ya msingi,
Rwamukwaya Olivier , katibu wa serikli katika wizara ya elimu, mjibika wa mashuli ya kiufundi na Odette Uwamariya, katibu kudumu katika wizara ya sheria.

Pia Kagame anatarajia kupokea viapo vya magavana ambao ni Menyentwari Alphonse wa mkoa wa magharibi, Musabyimana Claude wa kasikazini, Kazayire Judith wa mashariki na Marie Rose wa kusini.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments