Rais Kagame amteua Rugwabiza kuwa balozi wa Rwanda katika UN.

Katika mabadiliko makubwa yaliofanywa jana jioni, Rais Paul Kagame amemteua Bi. Valentine Rugwabiza kuwa balozi wa Rwanda katika umoja wa mataifa.

Rugwabiza amechukuliwa nafasi ya Eugene Richard Gasana aliyefutwa kazini mwezi Agosti,10,mwakani huu.

Valentine Rugwabiza amekuwa akihudumu kama waziri katika wizara ya jumuiya ya Afrika mashariki (MINEAC), wizara iliyofutwa na kujumuishwa katika wizara ya viwanda na biashara ambayo inaongozwa na Francois Kanimba.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments