Miss Mutesi Jolly akutana na prof. Murenzi nchini Ufaransa.

Balozi Jacques Kabale, Miss Mutesi Jolly na Prof. Romain Murenzi

Miss Mutesi Jolly yuko barani Ulaya katika ziara ya kazi.

Kwenye makao makuu ya shirika kimataifa la elimu, sayansi na utamaduni i(UNESCO) aliyopo mjini Paris, nchini Ufaransa siku ya jumatatu, oktoba,03,2014, alikutana na mwenyekiti wa UNESCO, tawi la kuimarisha sayansi na kujenga uwezo, Profesa Romain Murenzi.

Jolly alikuwa na lengo la kumfafanulia mipango anayo ya kukuza elimu, kufundisha vijana na kuwahimiza kwenda shuleni. Kama Rwanda Back up inspiration inavyosema.

Rwanda Back Up Inspiration inasema kuwa Murenzi alimuahidi kufadhili mipango yake ili naye aweze kuchangia mtaji wake katika maendeleo ya nchi yake.

Huko ufaransa , Jolly alipata fursa ya kukutana na Jacques Kabare, Balozi wa Rwanda nchini humo na Firmin Matoko, naibu mwenyekiti wa UNESCO.

Baada ya ziara nchini Ufaransa, Mutesi Jolly anachukua mizigo kwenda Ubelgiji ambapo anapotarajia kukutana na balozi wa Rwanda nchini Ubelgiji na Miss wa nchi hiyo.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments