Gatsibo : mke auawa na houseboy

I P Emmanuel Kayigi, msemaji wa jeshi la polisi katika mkoa wa mashariki mwa Rwanda

Siku ya jumatatu ilikuwa hali ya majonzi makubwa mjini Kabarore, wilayani Gatsibo kufuatia kifo cha Gaudence Uwihoreye ambaye amekuwa mama wa watoto wawili.

Akihojiwa na mwanahabari, Inspekta wa polisi Kayigi Emmanuel, msemaji wa jeshi la polisi mkoani mashariki alithibitisha habari hii na kuongeza kwamba uchunguzi bado unaendelea ili kuhakikisha jinsi alivyouawa marehemu.

‘’mwili wake umechukuliwa hospitalini Kiziguro kwa uchunguzi wa maiti na sasa hatujapata matokeo kuhusu chanzo cha kifo chake. Inawezekana kuwa ameuawa kwani alikutwa amefungwa katika bafuni na kamba kuzunguka shingo yake.’’ Kayigi alisema.

Yeye aliongeza kwamba uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa yuko house boy aliyeajiriwa na familia huyu ndiye anayeshukiwa haya mauaji.

Mutabazi anashitakiwa kutenda haya mauaji na kuiba vifaa vya nyumbani na kuiba fedha kutoka.

Jumatatu ya jana asubuhi, Vedaste Nsanzimfura alitoka nyumbani mkewe akiwa hai na akaenda mashambani, akirejea aliambiwaa na mtoto wake mwenye umri wa miaka 4 kwamba kitu kibaya kilitokea kwa mama yake.

Huyu house boy wake alimwambia kuwa Gaudence alianguka chini na alimpeleka katika kituo cha afya kilichopo karibu nao.

Nsanzimana alikimbia kwenda kituo cha afya na akafika huko manesi wakamwambia kwamba hawana Gaugence katika kituo cha afya kisha Nsanzimana akarudi nyumbani.

Alipofika nyumbani , akamkosa houseboy lakini akatambua kwamba house boy alitoroka akiiba vifaa vya nyumbani na pesa.

Aliendelea kusaka kisha akautambua mwili wa mke wake katika bafuni.

Ingawa ya houseboy kutoroka, polisi inasema kwamba haijui vitambulisho kamili vya mtuhumiwa zaidi ya kujua jina lake tu.

Na IP Kayigi anashauri kila mtu kujua vitambulisho kamili vya mtumishi wake

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments