EAC haijatoa wazi sababu iliyofanya Burundi kukata uhusiano wa kibiashara na Rwanda

Waziri wa Rwanda ambaye ni mjibika wa kazi ya jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Valentine Rugwabiza anasema kuwa uamuzi wa kuzuia usafirishaji wa mazao ya kilimo kuja Rwanda uliochukuliwa na nchi ya Burundi ni kunyume na sheria ingawaje mpaka sasa mawaziri hawakuwa bado kukaa pamoja kwa kuuliza viongozi wa Burundi sababu iliyowafanya kuchukua uamuzi huo.

Siku kadhaa zilizopita, makamu wa pili wa Rais, Joseph Butore alionya raia wa Burundi kutouza tena mavuno ya kilimo katika Rwanda na aliwaonya kwamba yeyote atakayejaribu kusafirisha mazao yake nchini Rwanda atadhibiwa.

Baada ya nchi hiyo jirani kupiga marufuku hii biashara, Balozi Rugwabiza alisema kwamba uamuzi huo ni kinyume na sheria kwani kabla ya nchi kuchukua uamuzi kama huo nchi mwanachama wa EAC inapaswa kwanza kufafanua sababu na kuomba ruhusa.

‘’wao waliamua hivyo pasipo kuomba ruhusa wala kueleza sababu, vikitokea hivyo, nchi hutakiwa kutoa sababu ya kukata biashara. Kwa hiyo, mnaskia hivyo ni kinyume na sheria.’’ Balozi Rugwabiza alisema.

Rugwabiza anasema kwamba licha ya kuwa hakuna utafiti wa kina uliofanywa kuhusu athari za uamuzi huo, vinaonekana kuwa warundi ndio waliothirika vibaya kuliko wanyarwanda.

Aliongeza kwamba hadi sasa mawaziri wa EAC bado hawakukaa pamoja kwa kuomba Burundi kutoa wazi sababu iliyowafanya kuchukua uamazi kama huo ambao ni kinyume na sheria zinazodhibiti mataifa wanachama wa EAC.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments