Mugambage ndiye balozi wa Rwanda Sudani Kusini

Balozi Frank Mugambage ambaye ni balozi wa Rwanda nchini Uganda pia amepokelewa na Salva Kiir katika ikulu nchini Sudani kusini.

Katika sherehe iliyofanyika jumatano iliyopita, Kiir alipokea barua ya stakabadhi ya kuruhusu Mugambage kuwakilisha Rwanda huko Sudani Kusini ; kama taarifa iliyotolewa na Ubalozi nchini Uganda inavyosema.

Ubalozi husema kuwa Kiir alipokea ujumbe aliotumwa na Rais Paul Kagame na Balozi Mugambe alimuahidi kuimarisha urafiki baina ya nchi hizo mbili.

Akimkaribisha, Kiir alisema kuwa anashukuru vyovyote Rwanda inavyofanya kwa kuisaidia Sudani kusini ili iwe salama na aliongeza kwamba anatumaini kwamba Sudan Kuseni huenda ikawa kama Rwanda baada ya hali mbovu ya usalama.

Ubalozi wa Rwanda nchini Uganga unasema kwamba Mugambage ni balozi wa Rwanda nchini Uganda na Sudani kusini na ataendelea kufanya kazi katika ofisi yake aliyoko nchini Uganda.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments