Rwanda yahudhuria mazishi ya Shimon Peres, Israel

Rwanda imemtuma waziri wake wa mambo ya nje na ushirikiano, pia msemaji wa serikali ya Rwanda Bi Louise Mushikiwabo kwa kutoa heshima zao za mwisho wakati wa mazishi ya kiongozi shupavu wa Israeli marehemu, Shimon Peres, aliyefariki Jumatano wiki hii.

Shinon Peres aliyekuwa mara mbili waziri mkuu wa Israeli kabla ya kuwa rais atazikwa leo hii, ijumaa k katika maeneo ya makaburi ya kitaifa mlimani Herzl mjini Jerusalem.

Waombolezaji watajumuisha Rais wa sasa wa Marekani Barack Obama na Rais wa zamani Bill Clinton, aliyefanya kazi na Bw Peres katika mkutano wa mwafaka wa amani wa Oslo mwaka wa 1993.

Viongozi kadhaa wa Kipalestina pia watahudhuria mazishi hayo akiwepo Rais Mahmoud Abbas na mpatanishi mkuu wa zamani Saeb Erekat.
Itakuwa mara ya kwanza kwa Bw Abbas kuzuru Israel tangu 2010.

Maelfu ya Waisraeli walitoa heshima zao za mwisho kwa hayati Peres, ambaye maiti yake imekuwa nje ya majengo ya Bunge la Israeli, Knesset.

Polisi wa Israel wamesema maafisa 8,000 wanatumiwa kudumisha usalama.
Mazishi hayo ndiyo makubwa zaidi kuwahi kufanyika Israel tangu mazishi ya waziri mkuu Yitzhak Rabin, aliyeuawa na Myahudi 1995.

Bw Peres alifariki Jumatano baada ya kuugua kiharusi kwa muda wa wiki mbili

. Wageni wengine mashuhuri ambao watahudhuria mazishibya Shimon Peres :

 Barack Obama, Rais, Marekani

 Bill Clinton, rais wa zamani, Marekani

 Mwanamfalme Charles, Uingereza

 Boris Johnson, Waziri wa mambo ya nje, Uingereza

 Tony Blair, waziri mkuu wa zamani, Uingereza.

 Malcolm Turnbull, Waziri Mkuu, Australia

 Justin Trudeau, Waziri Mkuu, Canada

 Donald Tusk, Rais, Baraza la Umoja wa Ulaya

 Francois Holland, Rais, Ufaransa

 Joachim Gauck, Rais, Ujerumani

 Matteo Renzi, Waziri Mkuu, Italia

 Jenerali Nakatani, waziri wa zamani wa ulinzi, Japan

 Jawad Anani, waziri wa ngazi ya juu, Jordan

 Enrique Pena Nieto, Rais, Mexico

 Jens Stoltenberg, Katibu Mkuu, Nato

 Mark Rutte, Waziri Mkuu, Uholanzi

 Valentina Matviyenko, spika, bunge la juu, Urusi

 Mfalme Felipe VI, Uhispania

 Ban Ki-moon, Katibu Mkuu, Umoja wa Mataifa

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments