Sugira Ernest aanza kuzaa matunda DRC

Sugira Ernest aliyenunuliwa na AS Vita Club ya Jamhuri ya Demokrasia ya Congo ameshinda bao la kwanza katika mechi ya kwanza ya timu yake katika ligi kuu ya DRC.

Ernest alikanyaga nyasi za uwanja akichukua uwanja wa Mkongo Tady Etekiama Agiti aka Dady Birori.

AS Vita Club iliicharaza FC MK 3-0, Bao la kwanza lilipachikwa na Omar Sidibe katika dakika ya 26, Ernest Sugira katika dakika ya 76 la mwisho lilifungwa na Chiko Ikanga Mayimona katika dakika ya 90.

Hilo ni bao la pili linalofungwa na Mnyarwanda Sugira baada ya kununuliwa na AS Vita Club ,timu kandanda ya wakongo.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments