Dkt Mukankomeje afutiliwa mashtaka

Mahakama ya msingi ya Kagarama amechukua uamuzi wa kufuta kesi dhidi ya aliyekuwa mkuu wa taasisi ya kusimamia mazingira nchini Rwanda Dkt Rose Mukankomeje kama Redio Voice of America ilivyotangaza.

Bi Mukankomeje alishikiliwa mwezi Machi,30, mwaka huu, akishtakiwa kuvunja siri ya kazi, kuficha dalili za uhalifu na kumnenea serikali.

Katika mwezi Aprili, Mukankomeje alihukumiwa siku thelathini za kifungo lakini baadaye akaachiwa kwa muda baada ya kukata rufaa.

Mahakama ametangaza uamuzi wa kufuta mashataka jumatano ya jana wakati ilikuwa siku ya kumfungulia kesi kwa kina.

Mukankomeje amekuwa akishtakiwa makosa ya kihalifu aliyoyafanya katika mazungumzo ya simu ya mkononi na Bisamaza Prudence ambako Mukankomeje alimfichulia kwamba alikuwa anachunguzwa.

Mukankomeje anafutiliwa mashataka baada ya nafasi yake kuchukuliwa Bi Collette Ruhamya aliyekuwa makamu wake.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments