Mgombea aliyeungwa mkono na Rwanda katika uchaguzi wa mkuu wa Benki ya Dunia achaguliwa.

Rais Kagame akiwa na Jim Yong Kim katika kongamano la WEF lililofanyika mjini Kigali mwaka huu.
Mmarekani Jim Yong Kim amechaguliwa kwa mara nyingine tena bila kupingwa kwenye uongozi wa Benki ya Dunia kwa muhula wa pili wa miaka mitano, kama taarifa ya idara ya maendeleo inavyosema.

"Wakati nilijiunga na Benki ya Dunia mwaka 2012, kulikuwa na malengo mawili kabambe yaliyohitajika kufikiwa : kumaliza umaskini uliokithiri ifikapo mwaka 2030 na kukuza mafanikio ya pamoja," Kim alisema katika taarifa yake.

Wakati alipokuwa katika ziara ya kazi nchini Rwanda mwezini Agosti, Rais Patrice Talon wa Benin na Rais wa Rawanda Paul Kagame walitamka kumtaka Bw Kim achaguliwe katika wadhifu tena.

Rais Kagame alisema kuwa anataka Kim Yong achaguliwe kwani yeye ni mtu aliyechangia nguvu muhimu kwa kuisaidia benki ya dunia kutimiza ndoto za kuyasaidia mataifa mengi yakiwemo Rwanda kukua maendeleo.

Na Patrice Talon alisisitiza kwamba bila shaka Kim anastahili chiti cha uongozi wa Benki ya Dunia kutokana na uwezo na uchapa kazi wake.

Bw Jim Yong Kim alisema kwamba mabadiliko ya anga, ukimbizi na magonjwa ya milipuko ni changamoto kubwa ambazo hutazamiwa na Benki ya Dunia kwa kuzitafutia suluhu.

Bw Kim, mwenye umri wa miaka 56, alikua kiongozi wa Benki ya Dunia mwezi Julai 2012. Muhula wake wa pili unaanza Julai 1, 2017.

Bw Jim

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments