Rwanda yatoa salamu za rambirambi kwa Israeli baada ya kifo cha Peres

Waziri mkuu wa zamani wa Israel aliyewahi kuhudumu pia kama rais Shimon Peres amefariki dunia akiwa na miaka 93.

Serikali ya Rwanda imetuma salamu za rambirambi kwa Waisraeli baada ya kutangazwa kwa kifo cha Rais na waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo ya kiyahudi.

Bw Peres, ambaye alikuwa mmoja wa waliosalia kutoka kwenye kizazi cha wanasiasa waliokuwepo wakati wa kuundwa kwa taifa la Israel mwaka 1948, alihudumu kama waziri mkuu wa nchi hiyo mara mbili na mara moja kama rais.

Alishinda tuzo ya amani ya Nobel mwaka 1994 kwa mchango wake katika mashauriano yaliyopelekea kutiwa saini kwa mkataba wa amani kati ya Israel na Palestina mwaka mmoja awali.

Akitumia ukurasa wake wa twitter, Bi. Louise Mushikiwabo, waziri wa mashauri ya kigeni na ushirikiano, pia msemaji wa serika ya Rwanda, alisema kwamba Rwanda inawapa pole waisraeli katika hii hali ya huzuni na majonzi kubwa.

‘’Pole kwa familia na ndugu za familia ya Shimon Peres’’
‘’tumemkosa mtu aliyehudumu katika kila wadhifa mkuu .’’
Louise aliandika.

Shimon Peres alikuwa nani ?

• Alizaliwa 1923 Wisniew, Poland, eneo ambalo sasa hufahamika kama Vishneva, Belarus

• Alichaguliwa kwenye Knesset (Bunge la Israel) mara ya kwanza mwaka 1959

• Alihudumu katika serikali 12, mara moja kama rais na mara mbili kama waziri mkuu.

• Alitazamwa kama mpenda vita miaka yake ya awali - aliongoza mashauriano ya kuitafutia silaha Israel ilipokuwa bado taifa changa

• Alikuwa kwenye serikali iliyoidhinisha sera ya kujengwa kwa makazi ya Wayahudi katika maeneo ya Wapalestina yaliyotekwa na Israel

• Hata hivyo, alitekeleza mchango muhimu katika kupatikana kwa Mkataba wa Amani wa Oslo, mkataba wa kwanza kati ya Israel na Wapalestina, uliosema wangefanya juhudi "kuishi kwa amani pamoja".

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments