Rwezamenyo : Raia wanashutumu uongozi kutotekeleza sera ya elimu bure kama vilivyoandikwa katika vitabu.

Baadhi ya raia wanapoishi tarafani Rwezamenyo, wilayani Nyarugenge wanalalamika kuwa watoto wao wanafukuzwa shuleni wakati elimu ya msingi inasemwa kuwa ni bure.

Wazazi hao wanasema kwamba ingawa serikali ya Rwanda inasema kwamba elimu ya msingi ni bure, watoto wao wanazuiwa kusoma kwa sababu wazazi wamekosa uwezo wa kulipa faranga zinazoongezwa mwalimu kama ada ya mapongezi.

‘’juzi niliwakuta watoto watano ambao walikuwa wakirejea nyumbani, nikawauliza kwa nini wanarudi nyumbani badala ya kusoma, wao wakanijibu kwamba wamefukuzwa kwani hawakulipa ada ya shule. Sasa mnaona mtu ataweza kulipa bima na ada ya shule ?’’
Murenzi Naason(mzazi) alisema.

Mzazi mwingine ambaye ana watoto watatu wanaosoma mashule ya elimu ya miaka 9, alisema kwamba yeye ni maskini mno mpaka yeye hana uwezo wa kulipa ada ya mapongezi na aliongeza kuwa umaskini wake husababisha watoto wake kutosoma kwani yeye amekosa fedha hizo.

Katibu mtendaji wa Rwezamenyo, Mutarugera Dieudonne alisema kwamba wao hawakujui tatizo hilo na alibaini kwamba iwapo watoto walifukuzwa kwani wamekosa pesa, hilo ni kosa kwani ni knyume na sheria.

Mutarugera aliwaomba wazazi ambao wana watoto waliofukuzwa shuleni kuwarudisha shuleni na makosa hayo atazungumziwa baadaye.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments