Polisi yazindua mtambo wa‘’Speed Governor machine’’ ambayo unatarajiwa kuokoa maisha ya watu.

Jeshi la polisi limezindua rasmi matumizi ya mashini itwayo ‘’Speed Governor’’ inayowekwa katika magari ya umma kwa ajili ya kutafutia suluhu ajali zinazotokea na kusababisho vifo.

Mashini hii inadhibiti kasi ya gari ambapo kasi haiwezi kuzidi kilomita 60/saa.
CP George Rumanzi, mkuu wa tawi la kitaani, anasema kwamba hizi mashini zina uwezo kuanza kutumika.

Dkt Nzahabwanimana Alixis, katibu wa serikali ambaye ni mjibika wa usafiri wa umma katika wizara ya miundombinu, alisema kwamba mfumo wa ‘Speed Governor’ ulichaguliwa ili kuepuka kasi zaidi ambayo hunyooshewa kidole kuwa ni chanzo cha ajali zinazosababisha vifo vya watu wengi.

na aliongeza kuwa yeyote atakayejaribu kuharibu mashini hii , atachukuliwa adhabu kali.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments