RBC yashindwa kueleza makosa ya kifedha inayodaiwa mbele ya wabunge.

Theoneste Karenzi, makamu mwenyekiti wa PAC (kushoto) na Juvenal Nkusi ,mwenyekiti wa PAC
Jana, Sept, 26, 2016 ndipo kituo cha Matibabu nchini Rwanda chilihojiwa na wabunge, tume ya PAC, kuhusu makosa ya kifedha waliodaiwa na ripoti ya mkaguzi mkuu.

Ripoti ya mkaguzi mkuu ya mwaka 2014/2015 inaishutumu RBC utawala bovu , Rwf 12.7 bilioni zilizotumika pasipo nyaraka za kifedha na Rwf 1.7 bilioni zilizo potelea katika matumizi fujo.

Pia, RBC inatajwa kuwa miongoni mwa taasisi kubwa zinazotumia vibaya bajeti ya nchi ingawa ya kupewa zaidi ya Rwf 100 bilioni pesa za Kinyarwanda.

Akiulizwa na Juvenal Nkusi. Mbunge, kinachotakiwa kwa kuwa nyaraka zinazoonesha jinsi wanavyotumia pesa na kutumia vizuri fedha ili kuokoa bajeti na maisha ya watu wanaolalamika ukosefu wa matibabu.

Theoneste Karenzi, makamu mwenyekiti wa kamati iliyowakilisha RBC bungeni , alijibu kwamba wao wanakwenda kuhimiza viongozi kwenye viwango mbali mbali kujibika matumizi ya fedha walizopewa.

‘’ ndio, kuna makosa ya nyraka za kifedha na makosa ya usimamizi wa hisa ya madawa, kosa lililosababisha hasara ya Rwf 405 milioni , hayo haendi kutokea tena.’’ Alisema.

Obadia Biraro, mkaguzi mkuu, aliambia PAC kwamba kuna makosa yaliotokea katika kituo cha matibabu ambako alisisitiza juu ya kosa la ukosefu wa umakini katika taarifa za kifedha.

Kwa kumjibu, James Kamanzi, mmoja wa wakurugenzi wa RBC, alikubali kosa la uzembe lakini alibaini kuwa hilo si kosa kwa taasisi yote, alisema kuwa linawezekana kuwa ni kosa lililotukia katika idara moja na aliwakumbusha kwamba kuna sehemu zilizofanya vizuri.

Hatimaye , wabunge na Mkaguzi mkuu waliishauri RBC kuwa ni bora kila idara kutekeleza majukumu yao vizuri hasa ya kifedha kisha wakaleta pamoja nyaraka zinazoonyesha jinsi kila idara hutumia bajeti ili kuwa na taarifa halali ya matumizi ya fedha na kuepuka makosa yanayotokea katika taasisi hii ya serikali inayosemekana kuwa miongoni mwa taasisi zinazotumia bajeti nzito.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments