Waziri nchini Uingereza awasili Rwanda

Waziri wa Idara ya maendeleo Kimataifa (DFID) Nchini Uingereza, James Wharton amefika salama nchini Rwanda katika ziara ya kazi.

Baada ya kuwasili, James amekwenda Musanze ambako atakutana na Gavana Bosenibamwe Aimee wa Mkoa wa kasikazini, Mameya, kama vile kuitembelea miradi inayofadhiliwa na Uingereza kama maafisa wa ubalozi wa UK walivyosema.

Pia huko Wilayani Musanze, Wharton analenga kujionea jinsi miradi ya VUP ilivyonufaisha wananchi na kukitembelea kiwanda cha viazi.

Mapema, Balozi wa Uingereza nchini Rwanda alisema kwamba ziara hii italenga shughuli zinazotekelezwa kwa ushirikiano wa nchi mbili kwa ajili ya kupungua umaskini, kuboresha elimu, biashara na uwekezaji.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments